Kauli ya Serikali Kuhusu Gazeti la Tanzanite Lililomwandika Mange Kimambi

Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema  imewaita wahusika wa gazeti la Tanzanite ambalo limesambaa mitandaoni likiwa limebeba katika ukurasa wa mbele habari inayomhusu Mange Kimambi.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dkt Abbas amesema kuwa, amelazimika kuwaita wahusika hao ambao atakutana nao leo ili aweze kusikiliza upande wao baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma ya gazeti hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad