Kwa mujibu wa gazeti la The Star limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia maeneo ambayo vyama vya upinzani nchini humo vina nguvu zaidi na kuendelea maeneo mengine.
Gazeti hilo limeripoti kuwa ziara hiyo itaanzia jimbo la Nyanza ingawaje tarehe rasmi ya ziara hiyo bado haijatangazwa.
Wakati hayo yakijiri, viongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya leo Jumatatu wanatarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu mustakabari na muelekeo wa umoja huo.
Wiki iliyopita Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga alikutana na Rais Uhuru Kenyatta kwenye Ikulu ya nchi hiyo ambapo kwa pamoja walikubaliana kujenga nchi na kuweka mbali tofauti zao za kisiasa.
Haya sasa nyie mnaopenda maandamano kwa kufuata mkumbo mtaweka wapi sura zenu......na wale walo uwawa-vepe? Ama kweli, siasa ni mchezo mchafu, hauna rafiki wakudumu wala adui wakudumu......wanapogombana shika-jembe ukalime..........TAFAKARI
ReplyDelete