Baada ya hapo jana aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Softcare Diapers, mjadala umekuwa mkubwa ni kwanii mastaa wa kike Bongo hawapati fursa kama hizo.
Muigizaji Faiza Ally alihoji ni kwa nini mastaa wa Bongo hawajapata dili hilo badala yake akapewa mtu mwingine, Faiza alienda mbali zaidi kwa kusema Wakenya na Waganda hawezi kufanya kitu kama hicho.
Sasa Shamsa Ford amepigana na mtazamo wa Faiza kwa kueleza kuwa mastaa wa kike Bongo wamejiharibia wenyewe ingawa wanajulikana lakini si kwa upande ambao unavutia kibiashara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Naona tu watu wanalalamika kwanini madili yanawapita mastar wa bongo na wageni ndo wanapata nafasi hiyo. Mimi nina mtazamo tofauti kabisaa, kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikagua wenyewe kwanza, nina uhakika kila biashara ina condition zake na kila biashara inahitaji faida.
Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua STAR wa bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara, tusipinge ukweli sisi wenyewe baadhi ya wasanii tumevunja uaminifu kwa wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu. Unapozungumzia kuwa ambassador unazungumzia kubeba brand ya mtu, sasa ni nani anaetaka kuchafua brand yake ibebwe na mtu asieeleweka, swala sio kujulikana tu ila unajulikana vipi!?
Maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika.kikubwa tujifunze, swala sio kujulikana ila swala ni kuwa unajulikana vipi!? Watu wanakutambua kwa lipi kisha akili kichwani mwako .Ni vizuri tumeumia sasa tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika…Niliowakera mnisamehe tu lazima tuishi kwa kuambiana ukweli.
Soma Pia; Zari awanyoosha mastaa wa kike Tanzania, alamba dili nono Dar
Utakumbuka February 14 mwaka huu (Valentine’s Day) Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’.
Kimenuka! Dili la Zali Lawagombanisha Shamsa Ford na Faiza
3
March 29, 2018
Tags
nyie kweli wajinga kwa ni zari kazidi nini si mwanamke kama any mwanamkevhalfu wanasema kuwa wabongo kwa ajili ya uaminifu na matendo yetu matendo gani kwa ni tukinao hakai uchi situmuona hadi makalio yake mkanda wa ngono si ulikuwa mitandaoni kuweni na akili sio kujidharau wenyewe serelikali ni lazima ikemee kwanza ni wananchi jipendeni bwana muendele mbele
ReplyDeleteBAHATI YA MWENZIO USIILALIE MLANGO WAZI......utajutraaaaa
Deletewe are not talking abt bahati kila mtu na alivojaaliwa lakini how come atoke mtu frm uganda or wherever sio mwananchi wakati wananachi wako na warembo na ikiwa ni ku kaa uchi mbona wote wako sawa tu si tuna yaona watanzania amkeni
ReplyDelete