Kingu: Kutekwa na Kuuawa ni Jambo la Kawaida Bunge Lisiunde Tume ya Kuchunguza

Kingu: Kutekwa na Kuuawa ni Jambo la Kawaida Bunge Lisiunde Tume ya Kuchunguza
MBUNGE wa Singida Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amedai kuwa vitendo vya watu kutekwa na kuuawa ni jambo la kawaida huku akilishauri Bunge kutounda Tume kuchunguza kwani itazua taharuki na Serikali haijashindwa kusimamia usalama wa nchi na raia wake.

Kingu amesema kuwa, matukio ya kihalifu yapo kila utawala na hakuna Taifa linaloweza kwenda bila ya kuwa na uhalifu.

Kauli yake inakuja wakati Taifa bado liko kwenye sintofahamu kuhusu kutekwa nyara kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu, kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu, Azory Gwanda, Ben Saanane, Salma Said na mauaji Alphonce Mawazo, Daniel John na Godfrey Lwena na mauaji ya wananchi wilayani Kibiti, Rufiji, Mkuranga- Pwani.

Kauli ya Kingu imekuja kama majibu kwa Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe aliyewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha Hoja Binafsi ya kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad