Kingu: Serikali Haijashindwa Kusimamia Usalama

Kingu: Serikali Haijashindwa Kusimamia UsalamaMbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema suala la bunge kujadili hali ya usalama wa nchi na kutaka kamati iundwe kuchuguza matukio ya kihalifu kutasababisha taharuki ambayo tafsiri yake ni kama serikali imeshindwa kusimamia usalama.


Mbunge Kingu ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na www.eatv.tv kuhusu kuunga mkono maamuzi ya Hussein Bashe ya kupeleka hoja binafsi bungeni kuhusu kuteuliwa kwa kamati teule ya kuchunguza matukio ya utekaji, mauaji na kushambuliwa kwa watu mbalimbali nchini.

Mh. Kingu amesema kwamba kwa upande wake anaamini kuwa Serikali haijashindwa kabisa kulinda usalama wa nchi mpaka suala hilo likajadiliwe ndani ya bunge na kusisitiza matukio ya kihalifu yapo nchi nyingi duniani na hata katika tawala zilizopita.

Akiendelea  kutoa ufafanuzi Mh. Kingu amesema kwamba anaamini Usalama wa nchi ya Tanzania upo vizuri kuliko hata mataifa mengine makubwa hivyo ni vyema pia kuangalia Tanzania inafananishwa na nchi gani katika kuangalia hayo matukio ya kihalifu  yanayotajwa.

"We must be smart kwa lengo la kuwa wazalendo kwa nchi yetu na hata serikali ikikosea tunapaswa kuikosoa na siyo kuibebesha mzigo. Lakini kwa vile ni hoja ya Mbunge mwenzangu naheshimu, sina mamlaka ya kuzuia wala serikali haina mamlaka  hivyo nasubiri ikifika bungeni tutaijadili na hata mimi nikipata nafasi nitachangia,"Mh. Kingu.

Pamoja na hayo Mh. Kingu amesema kwamba "Polisi wengine  wanakuwa hawana maadili lakini siyo kwamba serikali imeshindwa mpaka tuanze kuijadili na kuiwajibisha serikali. Jeshi la polisi l;iwe na utayari wa kutoa taarifa za haraka. Hii ni changamoto pia kwa jeshi la polisi na serikali.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bashe ni msaliti siku nyingi tu CCM na sijui wanmuekea nini kule CCM Wangemtimua tu aende kumfuata Lowasa kule Chadema . Anachokifanya Husein Bashe sio Demokrasi kama anavyojinasibu bali ni kuendeleza ughasi na kukiuka misingi ya uongozi na demokrasia ndani ya chama chake. Kama anadi maaumuzi na kauli zake zinasukumwa na demokrasia? Ninavyofahamu mimi demokrasia ni maamuzi ya wengi na Bashe sio independent politician bali yupo chini ya mamlaka ya CCM Sasa vipi achukue hoja ilokuwa serious kama Usalama wa taifa aifanye kuwa hoja yake binafsi bila ya kushauriana na wanachama wenzake kwanza ndani ya vikao vyao vya chama kabla ya yeye kuamua kujiripua kwenye vyombo vya habari?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad