Kiongozi wa ACT-Wazalendo Aliyepinga Waraka wa Maaskofu Avuliwa Uanachama

Kiongozi wa ACT-Wazalendo Aliyepinga Waraka wa Maaskofu Avuliwa Uanachama KioKiKKKKKKngozi wa Ngome ya Vijana ambaye ni Mratibu wa Masuala ya Elimu wa chama cha ACT-Wazalendo, Philipo Mwakibinga amevuliwa uanachama na chama hicho kutokana kupinga tamko la Maaskofu wa KKKT ambalo chama hicho kinaunga mkono.


Chama hicho kimesema amekuwa akitoa taarifa zinazokinzana na misimamo ya chama na kutolea mfano pia wakati wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin ambapo chama kimesema alitoa tamko ambalo lilikuwa kinyume na msimamo wa chama.

Mwakibinga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka WARAMI, aliupinga waraka huo kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

ACT Wazalendo kupitia kwa Katibu Uenezi wa Ngome ya Vijana, Karama Kaila kimesema kuwa kama hajaridhika na uamuzi huo anaweza kupeleka suala lake katika kamati ya maadili ya chama hicho ili liweze kushungulikiwa zaidi
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna ubaya gani kwa mwanachama kupingana na wazo la mtu wa tatu?
    ACT Wazalendo kwani nyie ndio mliotoa waraka?
    Kama hamkushiriki kuutoa, je kulikuwa na haja gani kila mwanachama wenu kuuunga mkono?
    Ah, nyie si ndio mnaopita kulalamika kuwa demokrasi inaminywa Tanzania?
    Sasa ikiwa demokrasi maana yake ni uhuru wa kutoa mawazo, vipi mumshurutishe kiongozi kukubaliana na wazo la mtu wa tatu yaani third person?
    Si siri kwamba hata kiongozi mkuu wa Katoliki Pelicarp Pengo ametofautiana na waraka wa maaskofu wake. Sasa nyie mna nini lakini?
    Au ni nyie mlioutayarisha ule waraka kisha mkaupenyeza kwa maaskofu wakusemeeni?
    Halafu eti nanyi mwajidai mnapigania demokrasi!!
    Hamna cha demokrasi wala haki. Ni ubinafsi tu niuonao hapa, kila mmoja kuvutia kamba upande wake.
    Ila muelewe kuwa mnahatarisha uhuru na amani ya nchi nzima.
    Walimchojoa Zito Kabwe kule kyadema, na sasa huyu nae anachojolewa kwa sababu zinazofanana.
    Mnamalizana wenyewe kwa wenyewe. Ndizo siasa za upinzani hizo. Urongo urongo na ubinafsi tu.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad