Yanga Jumanne itavaana na Township Rollers ya nchini Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam inaingia katika michuano hiyo ikiwa na alama 40 baada ya michezo 19 ya ligi.
Kocha huyo anayeinoa Dodoma FC kwa sasa alisema; “Yanga sio mbovu kama wengi wanavyodhani kama wangekuwa wabovu wasingekuwa wanapata matokeo kwenye mechi za ligi lakini ukweli ni kwamba wachezaji wake wamechoka ndiyo maana timu inaonekana kama imefulia.”
“Lakini kiukweli Yanga inapitia wakati mgumu lakini bado wachezaji wake wanapambana na wamekuwa wavumilivu naamini hata kwenye mechi za kimataifa watafanya vizuri tu wakipambana ingawa wapinzani wao wale wanaonekana wamewekeza sana kwenye soka.
“Sema kinachowamaliza ni kule kuchoka, Yanga haijapumzika msimu uliopita ligi imeisha Yanga ikaendelea na mechi za kimataifa imetoka hapo kidogo ligi ikaanza, katika ligi wachezaji wake asilimia kubwa wakaenda timu ya taifa kwenye michuano wanarudi ligi inaendelea ndiyo maana wamekuwa na wakati mgumu sababu hata mashine zenyewe zinachoka wakati mwingine.”
STORI: MARTHA MBOMA