KRC Genk yala Kichapo, Samatta Atokea Benchi

NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jioni ya leo ametokea benchi timu yake KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 nyumbani na KAA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjin Genk.

Samatta aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero katika jitihada za kocha Mbelgiji Philippe Clement kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji wasawazishe mabao, mara baada ya Gent kufunga la pili.

Mabao ya Gent yalifungwa na Birger Verstraete dakika ya 11 na mshambuliaji Mnigeria Samuel Kalu dakika ya 77 na baada ya Samatta kuingia, Genk ikapata bao moja, lililofungwa na Leandro Trossard dakika ya 87.

Samatta leo amecheza mechi ya 78 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Maehle, Seck, Writers/Wouters dk45, Pozuelo/Samatta dk77, Ndongala/Trossard dk70, Buffalo na Karelis.

AA Gent; Kalinic, Gigot, Rosted, Verstraete, Chakvetadze/Kubo dk61, Yaremchuk/Janga dk23, Kalu/Christiansen dk80, Asare, Simon, Foket na Esiti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad