Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkuyuni jijini hapa amesema wasimamizi na afisa misitu waliopo kituo cha Usagara wamekuwa wakiwanyanyapaa wauza mkaa ikiwa ni pamoja na kuwanyang'anya mkaa, na kisha kwenda kuuza kwa bei chee kwa maslahi yao binafsi.
"Afisa misitu wamekuwa wanawanyanyasa wauzaji wa mkaa kwa kuwakamatia mkaa na kutaifisha baiskeli zao kisha kuuza wao kwa bei ya chini kinyume na taratibu", alisema Mabula.
Pia amewataka wauzaji wa mkaa wadogo, kumfikishia taarifa katika ofisi yake pindi wanapokamatiwa mkaa na ikiwa na kutaifishwa baiskeli zao, ili wawafikishe mahakamani wakajibu vizuri.
Wauza mkaa hao wanaosafirisha mkaa kutoka vijijini mpaka mjini kwa kadirio la mwendo wa kilomita 120, wamemshukuru mbunge kwa kuwapa wepesi kwani wamekuwa wakikamatiwa baiskeli na mkaa pamoja na faini kubwa ambayo haitolewi risiti.
Kwa Mujibu wa Sheria za