LHRC Wampinga Waziri Nchemba Matumizi ya Viboko Shuleni

LHRC Wampinga Waziri Nchemba Matumizi ya Viboko Shuleni
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetofautiana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba ya kutaka walimu kutumia adhabu ya fimbo kuweka nidhamu kwa wanafunzi shuleni

Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dk. Nchemba alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi, ili kutengeneza hatima ya nchi.

Alisema wakati walimu wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kunyoosha nidhamu kwa wanafunzi kwa kutumia fimbo, wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwalalamikia na kuwataka wawaache watekeleze majukumu yao.

“Wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi, wapo watu wengine huwalalamikia tu, na hawajui kwamba kinachofanyika ni kwa manufaa yetu.

"Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo, ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk. Mwigulu.

Akizungumzia kauli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo Bisimba, amesema kutumia fimbo kwa mwanafunzi hakuwezi kusaidia kumjengea nidhamu.

Pia, amesema kutumia adhabu hiyo kunaweza kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao kielimu.

“Ni kweli kwamba walimu wanapaswa kuachwa watekeleze majukumu yao bila kuingiliwa, lakini linapokuja jambo la adhabu au kujenga nidhamu kwa wanafunzi lazima uangaliwe mfumo unaotumika,” alisema Dk. Kijo Bisimba na kuongeza:

“Zipo adhabu ambazo mwanafunzi anaweza kupewa akikosa, lakini si kwa kuchapwa fimbo. Unaweza ukafikiri ukimchapa ndio unamjenga, lakini kumbe ndio unambomoa zaidi.

"Nasema hivyo kwa sababu unapoanza kumchapa mwanafunzi hawezi kufanya vizuri tena darasani. Mimi namuomba waziri a-deal (ashughulike) na mambo ya wizara yake, ya elimu ayaache.”
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Adhabu ya fimbo inafaa ila iwekewe utaratibu maalum, isiwe km kumkomesha mtoto kwa influence ya chuki, hasira nk. Niliwahi kusikia majadiliano ktk nchi zilizotokomeza Adhabu ya kuchapa watoto, wakilaumu kuongezeka kwa utovu wa nidhamu na kuhoji kama utaratibu wa miaka ya zamani ya viboko kwa watoto urudishwe. Maandiko matakatifu yanatuonya tusiwanyime watoto mapigo.

    ReplyDelete
  2. Hata sisi tulikuwa wanafunzi enzi za viboko, binafsi viboko havikuwahi kuleta any negative impact kwenye capability yangu kimasomo. Ila viliwahi kutuhimiza kufuata utaratibu wa shule. Ila pia nilushuhudia mwalimu akinichapa kinyume na sharia za shule na mara nyingine kwa hasira. Lakini ukimchapa mtoto anza kumweleza kwanini umeona umchape. Anapofanya vizuri mfumo wa kutoa zawad au pongezi mbele ya watoto wote au wawazi uandaliwe kwa mtoto ili ku-motivate tibia njema

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad