Linah Afunguka Kuhusu Ndoa "Sipo Tayari Kufunga Ndoa"

Linah Afunguka Kuhusu Ndoa "Sipo Tayari Kufunga Ndoa"
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama 'Ndege Mnana' amefunguka na kudai hayupo tayari kufunga ndoa na Shaban Mchomvu (mwanaume aliyezaa na Linah) kwa sasa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vitu vinavyowakwamisha kufanya hivyo.


Linah amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

"Suala la ndoa zito sana, sina maana nakataa kuolewa na mzazi mwenzangu ila mambo ya ndoa sio ya kukurupuka japo natamani kuolewa kwa kuwa mimi ni mtoto wa kike, lakini sidhani kama nipo tayari kwa sasa hivi kuolewa. Mungu atusamehe tu tunazaa nje ya ndoa. Suala la ndoa ni la kujipanga sana", amesema Linah.

Pamoja na hayo, Linah amedai hata mzazi mwezake anafahamu fika kitu ambacho kinawakwamisha kutimiza jambo hilo la ndoa kwa wawili hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad