Lulu Diva adaiwa kumtelekeza mtoto wake Kijijini


SIKU zote raha ya ubuyu hauchagui umri wa kuumun’gunya, shida yake usijisahau tu ukameza na mbegu zake! Ubuyu uliotua mezani ni wa msanii anayechipukia na mwigizaji wa Bongo Movies, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ wa kudaiwa kumtelekeza mtoto wake wa kumzaa kijijini kwao huko Handeni jijini Tanga.

MTOA TAARIFA AWEKA WAZI KILA KITU
Msambaza Ubuyu ambaye ni jirani wa msanii huyo alitiririka kuwa, Lulu alimzaamtoto huyo wa kike miaka sita iliyopita huko Handeni, lakini watu wengi hawajui kama ana mtoto mkubwa hivyo.

Ilidaiwa kuwa, hata mchumba wake wa sasa hajui kuhusu hilo na wala hapendi kabisa kuongelea kuhusu mtoto huyo.

“Ninavyokuambia, huyo Lulu alipozaa mtoto huyo alimwacha kwa mama yake muda mrefu sana yeye akaja Dar, lakini kamwe huwezi kumsikia akizungumzia mtoto wake huyo kwa mtu yeyote wala kusema kuwa alishawahi kuzaa,” alidai mtoa ubuyu huyo.

MTOTO ANAMUITA DADA
Mpashaji huyo aliweka wazi kuwa,kutokana na kulelewa na bibi yake kwa muda mrefu, kwa sasa mtoto huyo anamwita Lulu Diva dada nahuwa anamuona mara mojamoja hivyo hata akienda kijijini kwao hajui kama ni mama yake, jambo ambalo Lulu anapenda liwe hivyo.

“Huwezi kuamini, mtoto ameshasahau kabisa kama Lulu Diva ni mama yake badala yake anamuita dada na mtoto wake huyo ameshazoea kumuita hivyo na wala hajali lolote,” kiliendelea kudai chanzo hicho.

MSIKIE LULU MWENYEWE
Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Lulu Diva ambapo alipoulizwa kuhusu hilo la kuzaa na kumuacha mtoto kijijini kwako alifunguka kama ifuatavyo;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Lulu? Hivi mtoto wako anaitwa nani?

Lulu: Mtoto wangu anaitwa nani? Yupi huyo?

Ijumaa Wikienda: Si yule ambaye umeamuacha kijijini?

Lulu: Hiyo kali jamani… alafu kwa nini nizae nimuache kijijini?

Ijumaa Wikienda: Unaogopa kuonekana mzee?

Lulu: Hakuna kitu kama hicho labda wanamfananisha mdogo wangu kuwa ndiye

mwanangu.

Ijumaa Wikienda:

Watu wanasema ni kweli anakuita dada kwa sababu ulimwacha muda mrefu.

Lulu: Si kweli jamani huyo ni mdogo wangu…

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad