Lwaitama: Kuna Kikundi cha watu Kinaendesha Serikali. Rais Adhibitiwe..

Inabidi tutofautishe kati ya dhana tatu;

i) Dhana ya Maendeleo: Wananchi wanahitaji maendeleo, lakini maendeleo ni maendeleo ndani ya Uhuru. Sio Maendeleo wakiwa wanaswagwa kama mateka, vingnenvyo wangewatafuta Wajapani Wajerumani waje hapa wawapige bakora ili wawe na majengo. Wananchi wanataka maendeleo ya watu, maendeleo ya kupata uhuru zaidi.

ii) Dhana Dola: Je ni dola ya kuchukulia watu mateka au ni dola la wachi huru amabo wamelidhia mamlaka fulani kwa watu ambao wanafanya kwa niaba yao?.

iii) Dhana ya Chama: Chama ni kitu kinachoshawishi, ni chombo cha kushawishi watu sio cha kuwatisha. Sio chama kinachosema usipochagua huyu maendeleo hayatakuja kwako, usipochagua huyu utashughulikiwa. Kikifanya hivyo sio chama tena bali chama dora. Ni kikundi cha watu kimekamata dola halafu kinatumia chama. Sio chama kuwashawishi watu bali kuwatisha kwa sababu watu wanataka kubaki hapo hapo walipo.

Hoja hapa ni kwamba ukishafika mahali ambapo chama kilichokuwa cha ukombozi, kimejigeuza kikawa chama Tawala "Sio mimi nasema ni wao wenyewe wanasema chama Tawala". Mimi nashangaa, baada ya kupata uhuru hakuna anayetakiwa kutawaliwa, aanatakiwa kuongozwa tu. Na kiongozi hawezi kutawala watu, anawaongoza tu kwa ridhaa yao.

Mkwaruzano hapa ni kupata katiba mpya ni katiba mpya inayopunguza mamlaka ya rais. INayoongeza nafasi ya wananchi wenyewe kusimamia mambo yao bila kutegemea mtu mmoja. Ni katiba ambayo yenye maudhui ambayo teuzi za rais lazima zipitishwe bungeni ziidhinishwe na watu wanaotokana na walichaguliwa. Iwe katiba ambayo mamlaka ya rais yanaweza yakahojiwa kutakapokuwa kumetokea uchaguzi. Mambo yote hayo ndiyo yanaitwa katiba mpya. Madai ya katiba mpya sio tu itangazwe kesho kwamba hii ni katiba mpya hapana, tunauliza ni maudhui gani? Je rais teuzi zake zimepunguzwa? Je Mihimili mingine uteuzi wake hauhusiani kabisa ba rais? Je Mamlaka imegatuliwa na Wilaya inaongozwa na watu waliochaguliwa?

Kenya inafanya hivyo, Mtu anayesima na kusema Wilaya fulani inahitaji kitu fukani ni mtu aliyechaguliwa na watu wa sehemu husika. Inayezungumza Wilaya ya Ireje inataka nini, awe ni mtu aliyechaguliwa na watu wa Ireje. Sio mtu aliyeteuliwa. Mtu aliyeteuliwa ni mratibu tu. Hiyo ndio maana ya katiba mpya. Katiba mpya sio neno. Watu wanadai.


Dhana ya maendeleo.

Kama watu wanataka kujiletea maendeleo sio kuletewa maendeleo na mtu. Wanataka nafasi ya wao kuamua leo tutachangishana hivi, kesho tutachangishana hivi, hela yetu ikichangishwa hivi itatumika kwenye hiki, hiki kitangoja kesho hiki kitangoja keshokutwa. Tunataka Katiba yenye maudhui hayo.

Tunataka katiba ambayo itapunguza uwezekano wa mtu mmoja au kikundi cha watu mahali kuwafanya wananchi ni mateka, watu ambao wanatafuta hisani. Yaani maendeleo ni hisani ambayo inatolewa na mtu akipenda. Yaani maendeo yanatolewa kama mtu amefurahi. Kutoka ngazi za juu mpaka ngazi za chini. Yaani na mkuu wa Wilaya na yeye anaweza akaamua.

Wananchi wananaandamana mbele ya Waziri mkuu wanasema ondoka na huyu mkuu wa Wilaya. Manake wamefika mahali huyu mkuu wa Wilaya ndie anawaamulia wanataka nini. Sasa wao wamepata uhuru miaka zaidi ya 50, walitegemea Mkuu wa Wilaya ni mtu ambaye ni Mratibu wa shughuli za Serikali. Ni mtu ambaye anawasikiliza wao.

VIDEO:

Dar Mpya/JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Linapokuja neno Mtanzania basi neno Mswahili ni neno halisi la kuelezea tabia za Mtanzania. Waswahili huwa na maneno mengi ya kujinasibu na kujifanya kujua kila kitu. Kwanza unapozungumzia uhuru na maendeleo unazungumzia vitu viwili tofauti. Hakuna nchi duniani yenye kudhibiti mienendo ya wananchi wake kisiasa kama China,hakuna maandamano,hakuna ya wananchi kuhoji chochote juu ya maamuzi ya wakuu wa nchi lakini kwa sasa unapozungumzia nchi vinara wa maendeleo duniani basi China vidume. Hata hao Korea kaskazini ambao wananchi wake hupangiwa mpaka wakati wa kulala hakuna nchi Africa nzima inayowapata kwa maendeleo. Hata hiyo South Africa wamepata maendeleo wakiwa katika hali ya kutawaliwa wakati nchi kadhaa Africa zikiwa huru zikiwa zinafurahia uhuru bandia wa wananchi wake kwani uhuru wa kweli kwa mwanadamu ni uhuru uliojengeka katika kuyatawala maisha yake kiuchumi. CCM ni chama tawala hata Chadema au CUF kikifanikuwa kushika Dola vitaitwa hivyo hivyo jina la chama tawala tena kuna hatari zaidi kwa chama kama Chadema chenye mwenyekiti wa maisha wa chama kushika madaraka katika nchi hii kwani neno chama tawala linaweza likawa halitoshi kwao wanaweza kuongezea chama tawala tukufu. Wakati mwengine inatia kichefuchefu unapoona baadhi ya mwanasiasa wetu au watanzania wanaojiita wasomi wakiisifia Kenya kuwa na mfumo mzuri wa kikatiba. Kenya ni miongoni mwa nchi za Africa zenye serikali corrupt huwezi kuifanananisha na Tanzania hata wakenya wenyewe wanatushangaa wanaposikia watanzania tunaisifia serikali yao. Kiuhalisia kenya ina maraisi wawili hivi sasa nchi gani yenye mfumo madubuti wa kikatiba inayoweza kuruhusu kutokea mambo kama hayo ya kiajabu? Watanzania wanataka maendeleo yatakayowafanya wafurahie maisha yao na familia zao na hahilisi kama kuna katiba mpya au la. Suala la katiba mpya ndio silaha pekee ya wapinzani kutafuta huruma ya kisiasa kutoka kwa wananchi hivi sasa. Suala la katiba mpya mwisho wa mjadala wake utaishia bungeni na kule bungeni CCM inanguvu ya kupitisha chochote kile wanachokitaka kwa hivyo watu waache kuropokwa hovyo kama vile wao ndio watunga sheria. Nnaamini Tanzania ipo katika kipindi cha mpito sawa na chuma ili kiwe imara zaidi lazima kipite kwenye moto. Hakuna katika historia ya Dunia nchi wananchi wake waliojitwala wenyewe bila ya usimamizi wa dola halafu nchi hiyo ikawa na mafanikio. Nnaimani kabisa na Magufuli ni mtu makini na mwenye kujiamini katika maamuzi hapaswi kusikiliza kelele za watu wanaotaka kumtoa kwenye mbio za ubingwa kwani kutokana uongozi wake thabiti Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye nafasi ya kuchukua ubingwa wa maendeleo Africa. Siku zote siwezi kusahau kauli ya nasaa muruwa ya kwake yeye mwenyewe Magufuli aliposema ukimuona adui anakusifia basi hupaswi kufuhia pongezi zake, kajifungie ndani na kutafakari kwanini?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad