Makamo wa Rais wa Zambia Ahukumiwa Kwenda Jela Baada ya Kuvamia Kituo cha Utangazaji

Makamo wa Rais wa Zambia Ahukumiwa Kwenda Jela Baada ya Kuvamia Kituo cha Utangazaji
KIONGOZI wa chama wa Chama cha Movement for Multiparty Democracy (MMD) cha Zambia, Dr Nevers Mumba, ametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kutoa habari za uwongo kwa ofisa wa polisi.

Dr Mumba ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais wa Zambia, amefutiwa shitaka jingine ambalo alikuwa akikabiliwa la kupita eneo kwa dhamira ya kufanya uhalifu.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Lusaka, David Simusamba, alimtia hatiani na kumhukumu Dr Mumba kifungo hicho cha miezi mitatu na kumpa fursa ya kukata rufaa mnamo siku 14.


“Nimeusikiliza upande wa utetezi wa Mumba kwa masikitiko na kwa maoni yangu ni kwamba kwa vile mtu huyo aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri na mtu maarufu, angejizuia kufanya aliyofanya. Hivyo namhukumu mhalifu huyo kwenda jela miezi mitatu tangu leo na anaweza kukata rufaa mnamo siku 14,” alisema Hakimu Simusamba.

Maelezo katika shitaka la kwanza yanasema Dr. Mumba, mnamo Novemba 8 mwaka jana, alitoa habari za uwongo kwa ofisa wa polisi Gladson Mwanza kwamba alikuwa na ahadi ya kukutana na mhariri wa shirika la Taifa la Utangazaji la Zambia (ZNBC).

Katika shitaka la pili, Dr Mumba akishirikiana na watu wengine, aliingia bila kibali chumba cha habari cha ZNBC kwa nia ya kuwatisha na kuwabugudhi wafanyakazi wa shirika hilo siku hiyohiyo.

Dr Mumba anadaiwa pia kwamba siku hiyohiyo aliyovamia chumba cha habari cha ZNBC alitoa vitisho kwamba angehakikisha kuapishwa kwa Rais-Mteule, Edgar Lungu, kusingefanyika.

Anadaiwa pia kusema kwamba ZNBC na wahariri wake walikuwa wanalipotosha taifa.
Hakimu Simusamba alisema baadhi ya mashahidi walithibitisha kwamba Dr Mumba alitumia maneno ya kabila la Kibemba ambayo yakitafsiriwa yana maana ya kutishia au kudharau.

Alisema maofisa wa polisi waliopochunguza suala hilo, waligundua kwamba Dr Mumba hakuwa na ahadi ya kukutana na mhariri yeyote wa ZNBC.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad