Klabu ya Manchester City Jana usiku imekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Fc Basel kwenye mchezo wa Marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya.
Magoli ya FC Basel yamefungwa na Elyounoussi na Lang huku goli la Man City likitupiwa na Gabriel Jesus.
Licha ya kupoteza mchezo huo Man City imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa tofauti ya goli 5-2.
Mchezo mwingine uliochezwa Jana ni kati ya Tottenham Hotspurs na wakongwe Juventus ambapo Spurs wamekubali kipigo cha goli 2-1 nyumbani na kutupwa nje ya michuano.
Spurs walikuwa wa kwanza kuona lango la Juventus kupitia kwa Son na baadae goli hilo kusawazishwa na Higuain kabla ya kinda wa Argentina Dybala kupigilia msumari wa ushindi.
Spurs imekuwa timu ya nne kuaga michuano hiyo yenye msisimko zaidi duniani baada ya FC Porto, Basel na PSG ambao nao walitolewa kwa kukubali kipigo nyumbani kwao .