Hii ni mechi ya Ligi Kuu England maarufu kama Premier League, ambayo kwa msimu huu wa 2017/18, ambapo mshindi wa leo atatoa nafasi ya pili kwa yeyote yule.
North West Derby kwa mara ya kwanza ilichezwa Aprili 28, 1894, katika mechi ya kirafiki kuelekea msimu wa ligi wa 1893/94, ambapo Liverpool ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Man United ambayo wakati huo ilikuwa ikiitwa Newton Heath.
Timu hizi mbili ndizo ze nye rekodi ya kutwaa mataji mengi ndani na nje ya England kwani kwa pamoja zina mataji 38 ya ligi kuu (mengine kabla ya mfumo wa sasa), mataji nane ya Europa Cup, mataji manne ya Uefa, mataji manne ya Uefa Super Cup na mataji 19 ya Kombe la FA.
Mataji mengine ni 13 ya Kombe la Ligi, moja la Klabu la Fifa, moja la Intercontinental na 36 ya mataji ya Ngao ya Jamii.
MTU AKIPIGWA ANASHUKA
Kwa sasa katika ligi kuu, Man United ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 62 huku Liverpool ikiwa nafasi ya tatu na pointi 60. Man City wao wapo kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 78. Timu zote zimecheza mechi 29.
Kama zikitoka sare, hali itabaki kama ilivyo lakini Man United ikishinda itajiimarisha katika nafasi yake ila ikitokea Liverpool ikashinda itakuwa imepanda hadi nafasi ya pili kwani itafikisha pointi 63.
Liverpool akipoteza atajiweka kwenye nafasi ngumu kwani atabaki na pointi 60 huku Tottenham Hotspur mwenye pointi 58 kama akishinda atapanda nafasi ya tatu kutoka nafasi ya nne.
LIVERPOOL FOWADI KIWEMBE, BEKI NYANYA
Safu ya ushambuliaji ya Liverpool ina mabao 67 hadi sasa ambayo ni 11 zaidi ya yale ya Man United ambayo
ni 56, hii ina maanisha kwamba safu yao ya ushambuliaji ina y oongozwa na Mohamed Salah n i kali kuliko ya M a n United iliyo chini ya Romelu Lukaku.
Licha ya fowadi ya Liverpool kuonekana kuwa bora, beki yake ni nyanya kwani imeruhusu mabao 32 huku ile ya Man United ikiruhusu mabao 22 tu ambayo
ni kumi pungufu ya yale ya Liverpool. Hivyo, katika mchezo huu Liverpool inaweza kupata mabao hata mawili lakini nayo inaweza kuruhusu mabao kama hayo.
Man United nao safu yao ya ushambuliaji haiaminiki sana ila inaweza kubadili matokeo muda wowote ule kwani wachezaji kama Lukaku, Paul Pogba, Jesse Lingard, Anthony Martial na Marcus Rashford wapo vizuri.
Virgil van Dijk, Dejan Lovren na Nathaniel Clyne wanaonekana bado hawana uwelewano mzuri katika beki ya Liverpool kama ilivyo kwa Victor Lindelöf, Chris Smalling na Phil Jones wa Man United.
HAPA SALAH PALE LUKAKU
Licha ya Salah wa Liverpool kufikisha mabao 24 katika ligi kuu hadi sasa huku Lukaku akiwa na mabao 14, hiyo haiwezi kufanya Lukaku aonekane si lolote mbele ya Salah.
Wawili hawa watatazamwa zaidi kwa kila upande katika kuhakikisha ushindi unapatikana h a s a u k i l i n g a n i s h a n a mechi z a o zilizopita.
Salah amecheza mechi 28 na kufunga mabao 24, akiwa amepata ushindi mara 16, kufungwa mara tatu, lakini ametoa asisti nane na amepiga pasi 758, huku akiwa ametengeneza nafasi 10.
Amepiga krosi 64, na kati ya mabao 24 aliyofunga kwa kichwa amefunga mara moja, mguu wa kulia mara mbili na k u s h o t o mara 21 na mara moja kwa penalti.
Lukaku yeye, katika mabao yake 14, amecheza mechi 28 na kupata ushindi mara 18, kafungwa mara tano, ana asisti sita, amepiga pasi 618, ametengeneza nafasi saba huku akipiga krosi 28.
Kati ya mabao 14, Lukaku amefunga matatu kwa kichwa, mawili kwa mguu wa kulia na tisa kwa mguu wa kushoto akiwa hana bao la penalti wala la faulo.
MOURINHO, KLOPP ANA KWA ANA
Wote ni makocha wenye ujuzi wa hali ya juu, lakini wamezidiana mbinu za kimchezo kwani Kocha wa Man United, Jose Mourinho ni mzuri katika kuzuia kwani akipaki basi ni ngumu kumfunga.
Wakati Mourinho ni mjuzi wa ulinzi, katika ushambuliaji anaonekana si mzuri sana mbele ya Liverpool ndiyo maana ana mabao 56 wakati Liverpool inayo 67.
Klopp yeye ni mzuri katika kushambulia lakini mbovu katika ulinzi ndiyo maana timu yake inapata mabao mengi pia inaruhusu mabao mengi, kwa hiyo mechi hii ni tamu kuitazama.
Mechi ni tamu sababu inazikutanisha timu zenye makali katika maeneo tofauti, Liverpool ushambuliaji, Man United ulinzi japokuwa wakati mwingine inakuwa nyanya.
MAN UNITED KIBOKO
Katika mechi 51 walizocheza hadi sasa katika mfumo wa sasa wa ligi kuu, Man United imeshinda mara 27 huku Liverpool ikishinda mara 13 na timu hizo zimetoka sare mara 11.
Kati ya ushindi wa mara 27 wa Man United, mara 15 imeshinda nyumbani na 12 ugenini wakati Liverpool mara nane imeshinda nyumbani na tano ugenini.