Mbowe Awekwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari

Mbowe Awekwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari



Mdakatari waliokuwa wakichunguza maendeleo ya afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi wamemruhusu kuondoka hospitalini hapo huku wakimtaka awe chini ya uangalizi kutokana na maradhi yake


Mbowe ameruhusiwa kuondoka hospitalini hapo jana saa 1:30 usiku, akiwa ameambatana na mkewe Dk. Lilian Mbowe, baada ya madaktari wa hospitali hiyo kuridhishwa na afya yake kurejea katika hali ya kawaida.

Katibu wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema Mbowe aliondolewa KCMC na kwenda mapumzikoni nyumbani kwake Nshara, Machame, Wilaya ya Hai.

Kwa mujibu wa Lema, Mbowe ameshaondoka hospitali ya KCMC na sasa  yuko nyumbani kwake, baada ya madaktari kushauri akae mahali ambapo atapata muda mrefu wa kujitenga na kupumzika vya kutosha, mbali na kazi yake ili amalize dozi yake ya dawa alizopewa.

Alipotafutwa Ofisa Uhusiano wa Hospitali hiyo ya KCMC, Gabriel Chisseo kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo amekiri Mbowe kuruhusiwa kuondoka hospitalini hapo, baada ya madaktari kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai, alikuwa amelazwa katika Wodi ya Watu Mashuhuri (VIP), tangu Jumapili ya Machi 4, mwaka huu. Alipofikishwa hospitalini hapo saa 9:20 siku hiyo, aliwekewa mashine ya oxygen kwa azidi ya saa moja, huku ikielezwa pia kwamba alipopelekwa wodini kulazwa, vipimo vilionyesha shinikizo la damu kuwa juu ya wastani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad