Akiwa porini mbunge Rweikiza amesema kuwa amepokea kero nyingi za wananchi na kwakuwa ana silaha akaamua kushirikiana na wawindaji ili kuondoa wanyama hao na kuahidi kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu mpaka wahakikishe wanyama hao waharibifu wanatoweka.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa inawalazimu muda mwingine kushindwa kupanda mazao ya chakula kwa hofu ya wanyama huku wakiongeza kuwa ngedere wamefikia hatua ya kuingia kwenye nyumba zao na kula chakula ambacho tayari kimepikwa.