Mbunge Aongoza Wananchi Kuua Tumbili

Mbunge Aongoza Wananchi Kuua Tumbili
Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini Jasson Rweikiza kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wawindaji wameamua kuingia porini katika maeneo ya Kemondo wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuwaondoa Ngedere ambao wamekuwa kero kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akiwa porini mbunge Rweikiza amesema kuwa amepokea kero nyingi za wananchi na kwakuwa ana silaha akaamua kushirikiana na wawindaji ili kuondoa wanyama hao na kuahidi kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu mpaka wahakikishe wanyama hao waharibifu wanatoweka.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa inawalazimu muda mwingine kushindwa kupanda mazao ya chakula kwa hofu ya wanyama huku wakiongeza kuwa ngedere wamefikia hatua ya kuingia kwenye nyumba zao na kula chakula ambacho tayari kimepikwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad