Mchungaji mmoja kutoka Nigeria (39), Andrew Ejimadu wa kanisa la Christ Freedom Ministries amezua gumzo mtandaoni baada ya ku-post picha zake katika mtandao wa Facebook wakati wa kuabudu mitandaoni.
Nabii huyo ameshangaza maelfu ya watu baada ya kuonyesha picha za waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake akidai kuwa kwa kufanya hivyo watapata baraka na miujiza.
Nabii huyo aliweka picha hizo katika ukurasa wake na kuandika.“Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”
“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” Andrew Ejimadu.
Mwaka 2016, Mchungaji Ejimadu alipamba vichwa vya habari na kushikiliwa na polisi nchini Zambia yeye na kaka yake, Cleopasa Ejimadu kwa kosa la kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikwenda kwenye makazi yao kwa ajili ya uponyaji na kupata ushauri wa kiroho.
Mpekuzi
kicheko kikubwa hiki.kweli upumbavu.baraka anatoa Allah sio Mchungaji ,viatuvinapitia chooni halafu kunabaraka.HEBU FIKIRIENI
ReplyDelete