Mchungaji Moshi Akamatwa na Polisi Kwa Kudaiwa ni Mchochezi wa Kisiasa


MOSHI, KILIMANJARO: Mchungaji Fredy Njama wa Usharika wa Karanga, KKKT Dayosisi ya Kaskazini, amekamatwa na Polisi kwa kinachoidaiwa kuwa ni “Uchochezi wa kisiasa”.

Mchungaji huyo wiki mbili zilizopita alisoma ripoti katika mkutano mkuu wa mwaka wa usharika wake ambayo ndo imepelekea kukamatwa kwake.

Katika ripoti hiyo, alibainisha kuwa mapato ya usharika yanapungua kwa sababu mbalimbali

Katika utangulizi wa ripoti alitaja changamoto 6 zinazoikabili nchi kwa sasa: Ukosefu wa ajira kwa vijana, Hali ya uchumi inayoyumba, Hali ya kisiasa ni ya mashaka, Gharama kubwa za matibabu, Sera ya elimu bure na Wastaafu kutolipwa mafao yao

Ripoti hiyo pia imechapwa ktk kijitabu na kiwanda cha uchapaji cha Dayosisi hiyo

Kundi la Polisi na maafisa usalama walimchukua Ijumaa asubuhi hadi kiwandani na kumtaka akusanye vijitabu vyote hadi vilivyosambazwa na kuvikabidhi Polisi. Aidha walimtaka aandike barua kuomba radhi na kufuta ripoti hiyo

Jioni ya leo, Polisi walifika ofisi ya usharika na kufanya upekuzi. Walichukua laptop na flash. Kisha walimpakia mchungaji katika gari lao na kuondoka naye.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad