Wafanyakazi hao ni pamoja na Katibu wa Wafanyakazi wa Rais Donald Trump, Rob Porter na Mwandishi wa hotuba za Ikulu hiyo David Sorensen.
Sasa leo March 1, 2018 taarifa kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na mmoja wa washauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ajulikanaye kama Hope Hicks pia ametangaza kujiuzulu.
Hicks ameeleza sababu yake ya kujiuzulu ni kwamba, tayari ametimiza wajibu wake katika ikulu hiyo ya White House.