MWANAHABARI Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi kwa muda baada ya kudai amewakimbia aliowaita “wauaji” wake.
Ngurumo amethibitisha kuikimbia Tanzania ili kulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.
“Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai, ili kunusuru uhai wangu, nililazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako nimepewa hifadhi,” alisema Ngurumo.
Aliongeza kwamba hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni “hifadhi ya kimataifa,” kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.
Aidha, vyombo vya habari vya Finland na mitandao ya kijamii, vimeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.
“Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa,” amesema Ngurumo.
Kuna usemi wa kisukuma unaosema....Happiness will never come to those who fail to appreciate what they already have..Mtu kamwe hawezi kuwa na maisha ya furaha maishani mwake kama atashindwa kukithamini kile kidogo alichojaaliwa. Kuitukana na kuizulia uongo Tanzania na kwenda kujikweza kwa wazungu unadhni ni kutisua? Hapana time will tell and God will make you pay price for this. Katika hali ya kawaida mtu hawezi kukutishia kifo kama wewe mwenyewe binafsi hujazulumu watu. Yaani kuna kitu kinaitwa karma neno linaloamanisha yakuwa ukimtendea mtu ubaya basi ubaya huo utakurejea na kuja kukutafuna. Huyu mhariri hapana shaka alikuwa anatumia taaluma yake vibaya kwa kuwakosesha amani baadhi ya watu bila ya sababu na ataendelea kukosa amani kwani badala ya kutubu kaenda kutenda zambi za kudang'anya zaidi . Lakini huko aliko kama kafanikiwa kuwadanganya wazungu wakamuamini kuwa maisha yake yapo hatarini Tanzania lakini Mungu anamuona na hayo madai yake na hapana shaka yeyote kama ya kweli au la? Kwenda kuipaka matope nchi iliyokusimamisha kuwa wewe kama wewe laana zake huwa za milele. Ni miongoni mwa wasaliti mambo leo wa kikazi hiki cha siasa ya vyama vingi Tanzania. Hakuna isipokuwa ni uselfish uliompelekea kwenda kuitangaza Tanzania kuwa sio nchi ya amani. Yaani yupo tayari kuwajengea mazingira magumu watanzania wenzake walio kwa mamilioni ili mambo yake yaende. Nchi hii umejaa wasaliti hadi wanafika kujianika wenyewe kwenye mitandao. Mzalendo wa kweli hawezi kuwa COWARD akaikimbia nchi yake kwa visababu vya uzushi. Kama mtu alizoea kuishi kwa kuuza habari za uongo na kupandikiza chuki kwenye jamii basi mtu huyo hawezi kuwa na maaisha ya amani mpaka atakapoamua kutubu nakuomba radhi..lakini kitendo cha kuenda kuisaliti nchi mara nyingi huwa hakina msamaha.
ReplyDelete