Miguna Awaandikia Waraka Wakenya "Mipo Hai Lakini Nina Maumivu Makali"

Miguna Awaandikia Waraka Wakenya "Mipo Hai Lakini Nina Maumivu Makali"
Habari za asubuhi, mchana na jioni wazalendo wa Kenya na marafiki wa Kenya popote mlipo. Mimi niko hai. Namshukuru Mungu kwa hilo.

Lakini nina maumivu makali, msongo wa mawazo na usumbufu. Mkono wangu wa kushoto bado umevimba vibaya. Naamini majambazi ya Jubilee yalinidunga sindano ya IV kunifanya nisiwe na fahamu katika kipindi chote cha safari nikiwa kwenye ndege kati ya Nairobi na Dubai.

Upande wa kushoto wote unaniuma sana. Bado sijafanyiwa vipimo ili kubaini kemikali ambayo majambazi haya yalinidunga kwa nguvu na kinyume cha sheria Jumanne jioni.

Napenda kuwafahamisha mke wangu, watoto, familia, ndugu, marafiki, wafuasi wangu, wanaotutakia mema na wanachama wa vuguvugu la kundi la NRM kwamba nimetelekezwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.

Nawasubiri wanasheria wangu wawasiliane nami kuhusu amri za hivi karibuni zilizotolewa na mahakama na hatua gani wameshachukua au wanatarajia kuchukua ili kukazia hukumu.

Narudia kusema kwamba ni lazima tuhakikishe kwamba kila mtu, bila kujali ana mabavu au dhaifu kiasi gani, anaheshimu, anazingatia na kutii amri za mahakama na atende kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria!

Pili, mahakama zenye mamlaka zimetoa amri kwa serikali isiyohalali kunirejeshea au kunipa hati halali ya kusafiria ya Kenya. Nataka na ninatarajia amri hizo zitaheshimiwa kikamilifu.

Nasisitiza kwamba haki zangu za kikatiba za kuwa pasipoti ya Kenya ziheshimiwe na zizingatiwe.

Dk Miguna Miguna ashangaa amefikaje Dubai

Haki yangu ya kusafiri ndani na nje ya nchi kwa uhuru pia lazima iheshimiwe na izingatiwe wakati wote, katika namna ileile haki hizi zinavyotumika kwa Wakenya wengine.

Nasubiri kuruhusiwa na mamlaka za Shirika la Ndege la Emirates na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kupewa tiketi ya kurudi Nairobi.

Natarajia kurejea Nairobi kwa ndege mapema iwezekanavyo. Ni haki yangu ya kuzaliwa, kikatiba na kisheria pia. Sitaacha kudai haki zangu kwa sababu ya utawala wa kiimla na matakwa ya waliotwaa mamlaka kwa mabavu.

Nawataka wote tubaki imara, tuzingatie malengo na tusiogope. Hiyo ndiyo njia pekee kwetu sisi kujikomboa na kuikomboa Kenya kutoka kwenye makucha ya madikteta Jubilee pamoja na wasaidizi wao na washirika wao. Dk Miguna Miguna
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad