Mimi Mars Naye Afunguka Kuhusu Kuwa na Mtoto

Mimi Mars Naye Afunguka Kuhusu Kuwa na Mtoto
Baada ya Vanessa Mdee kusema kwa sasa hayupo tayari kuwa na mtoto, Mimi Mars naye pia amefunguka kuhusu hilo.

Mimi Mars amesema kupata mtoto au kuwa mama wa familia ni kitu ambacho wanakihitaji ila ni kwa kipindi cha mbeleni zaidi takribani miaka mitano ijayo.

“Mimi baada ya miaka mitano hivi itakuwa fresh, huku mbele anaweza nikawa mama mwenye familia labda nimeolewa Mungu akijalia lakini napenda sana watoto, napenda sana kuwa na familia na ninapenda kuwa mama familia, so hicho ni kitu kipo kwenye plan zangu,” Mimi Mars ameiambia Bongo5.

Vanessa Mdee na Mimi Mars ni mtu na dada yake na wote wanafanya kazi zao za muziki kupitia label ya Mdee Music pamoja na Brian Simba. Mimi Mars kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Papara’.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad