DODOMA: Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesema ni muhimu kuitishwa mjadala wa kitaifa ili kujadili hali ya elimu nchini
Amefafanua kuwa ni lazima taifa litafakari kwanini shule za serikali zinaendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kila mwaka
Aidha, Mkapa ameshauri mjadala huo uhusishe makundi yote ya jamii wakiwemo wadau kutoka sekta binafsi, wasomi pamoja na wananchi wa kawaida ili kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hilo
Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ameyasema hayo wakati wa tukio la kumkaribisha Makamu Mkuu mpya wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Egid Mubofu na kumuaga aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo aliyemaliza muda wake, Profesa Idrisa Kikula.