Katibu Mkuu wa Young Africans Sports Club, Charles Boniface Mkwasa ametangaza rasmi siku maalumu ambayo itafanya mkutano mkuu wa wanachama wote wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali muhimu ya maendeleo.
Muda mfupi uliopita Mkwasa ameiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.
Mkwasa ameongeza kuwa kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika jumapili iliyopita imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa baaadae.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Mei 5 mwaka 2018 jijini Dar es Salaam huku wanachama wenye kadi za aina zote mbili za zamani na zile zinazotolewa kupitia benki ya posta wataruhusiwa kuingia ukumbuni.