Mmiliki wa Facebook Aomba Radhi kwa Kashfa ya Kuingilia Data za Watimiaji wa Facebook


Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica,ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

AmesemaThe CEO said: "Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu,na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia,mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu."Amesema Zuckerberg.

Nini ambazo Zuckerberg ameahidi kukifanya?

Katika kufuatilia matatizo ya sasa nay a zamani amesema atafanya mambo yafuatayo


Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko yam waka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
Kufanyia uchunguzi kazi za program za kimitandao zinazotiliwa shaka
Kupiga marufuku mwanzilishi wa program yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zita pafanya Facebook kuwa mahala salama.


Mchambuzi wa BBC wa masuala ya kimitandao Dave Lee, BBC kutoka America Kaskazini,anasema kwamba kile anacho kiona ni Facebook kwamba hawapo tayari kuomba radhi kwa kile kilichotokea.

Na pia amesema hakuna maelezo yoyote kwa wizi wa taarifa zake uliofanyika mwaka 2014,hapo ilikuwa ni wakati muafaka kuchukua hatua sitahiki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad