Mnyama Mrefu Zaidi Duniani Amegundulika Kuwa Ana Sumu

Mnyama mrefu zaidi duniani amegundulika kuwa ana sumu
Wanasayansi kila kukicha wanafanya tafiti ili kugundua vitu vipya sasa leo March 31, 2018 imegundulika kuwa Mnyama mrefu zaidi duniani ana sumu.

Watafiti nchini Sweden wamegundua kuwa mnyoo wenye urefu wa Mita 55 ana sumu lakini sumu hiyo haina madhara yoyote  kwa binadamu.

Profesa wa chuo kikuu cha Uppsala nchini Sweden,Prof. Dr. Ulf Göransson wakati alipohojiwa na kituo che television cha taifa amesema kuwa  utafiti kuhusiana na minyoo inayoishi katika hali ya baridi nchini humo umeoyesha kuwa minyoo hiyo ina sumu.

Kwa mujibu wa habari taarifa iliyotolewa Sweden, inawezekaan siku za baadae minyoo hiyo inaweza kuja kutumika kutengeneza dawa.

Minyoo hiyo kwa lugha ya kirumi inaitwa “Lineus longissimus”,na ina urefu wa mita 55-60
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad