Mtangazaji Mamy Baby wa Clouds Awachana Basata na Naibu Waziri Kiana Kupitia Ndoto


Ameandika Mamy Baby - NDOTO ZANGU

"Uso Wangu Upo Katika Tabasamu Pana. Ni Ile Nyimbo Inayopendwa Na Wengi Naona Inapigwa Kwenye Kituo Kikubwa Cha Televisheni Duniani, Kwa Furaha Isiyo Kifani Napitiwa Na Usingizi Mororo. Ndoto Zinanijia, Ninaona Tour Za Akina Jay Z Zikiwa Hazikatiki TZ, mara Dar live, mara Mkwakwani Tanga. Taswira Nyingine Inakuja, Naona Tuzo 4 Za BET Kwa Wasanii Wa Bongo na Hall of Fame moja ya Grammy kwa Mkongwe wa Muziki Tanzania. Kuna Picha Za Wasanii 10 Zinapita Mfululizo Wakiwa Kwenye Magari Yao Ya Kifahari Ferrari Mpaka Lamborghini.... Nastuka Usingizini Na Kugundua Nilikuwa Kwenye Ulimwengu Wa Kufikirika, Ulimwengu Ambao Tanzania Haijaamua Kuufuata. Moyo wangu ghafla umefadhaika kwa sababu nilichoota naamini kinawezekana kutokea ila sioni dalli. Mawazo yangu yanapelekea nitume salamu za ndoto zangu kwa Mhe. Naibu Waziri, Juliana Shonza. . .


1. Nakusalimu Mheshimiwa, mimi mwanamke mwenzako ambaye Natamani kuona ukiacha alama kwenye sanaa yetu natamani uache LEGACY ya sisi kujivunia juu yako. Napata shida kufikiria mabadiliko ya BASATA yatakayoendana na kukutana na Teklonojia na mifumo ya kisasa itakayowezesha hata usajili ufanyike online, TUTAFIKA HUKO KWELI? .

2. Pokea Salamu hizi za kipekee, salamu zenye ndoto kubwa. Ndotoni nimeona wasanii wakilipwa vyema na COSOTA kwa nyimbo kupigwa redioni, wakitajirika kwa kupata haki zao miaka 30 toka waanze kupigania hilo jambo.. Naomba nifahamu ndoto hii, itatimia kweli? .

3. Salamu za kheri hizi Mheshimiwa, nimeota Roma Amemfunika Yule Cassper Nyovest Kwenye Show huko Marekani. Hivi Inawezekana kukawepo namna nzuri ya kudumisha urafiki wa wasanii na wizara na kanuni za kisasa ziwasimamie na kwa ukubwa wa wasanii wetu waalikwe Ulaya kuimba kwenye viwanja sio kwenye migahawa? .

4. Usichoke salamu zangu mheshimiwa, wale waliofungiwa kwa maadili ya Video za muziki wao, tunawaambiaje pale ambapo hatuwezi kufungia video za Rihanna zisichezwe nchini au kila mtu atoe nyimbo YOU TUBE tu ambapo watu wenye kipato cha chini wasiweze kuwa na haki ya kuona, tubaki sisi tu wenye kipato kidogo? .


5. Natamani kukusalimu kwa ukaribu zaidi lakini acha nizitume hapa, nakwambia kweli nimeota Wizara imeweza kufanikisha mazingira ya biashara kubwa ya muziki. Utaliwezesha vipi hili mheshimiwa litakusaidia sana kwenye kuondoka na Legacy ya hatari tutakayoikumbuka.... .

6. Kwenye Ndoto zangu nimemtizama Yule Kijana Aliyezoea Kwenda Kwenye Show za wasanii kama Leaders lakini muda umepunguzwa na Leaders yenyewe pamefungiwa. Utamsaidia vipi huyu naye aweze kuhadithia watoto wake kwani naona dalili za matamasha Dar es Salaam kupotea kabisa....bado nakusalimu tu Mheshimiwa. .

7. Ndotoni namwona bibi yangu, najiona mimi na wewe, namwona mdogo wangu na wanangu. Wote tuna hisia tofauti kwa wimbo mmoja, pokea salamu mheshimiwa. Kwani Maadili tunayajudge vipi? Huu wimbo wa maadili nani atamhadithia mwenzake???? .

8. Nisikuchoshe na Salamu Zangu Mheshimiwa, nakaribia mwisho wa simulizi ya ndoto zangu, nimeona Jay Z na Beyonce wapo bongo kwenye ukumbi mmoja wa maana.? .

9. Mwisho kabisa nimekuona Ndotoni ukikabidhi tuzo ambayo ina hadhi kubwa sana na unashangiliwa mno unaposhuka kwani sio tu umempa tuzo msanii mkubwa ila maandalizi yake yamefana sana kwa event hiyo kubwa iliyofanyika Mlimani city. .


Roho inauma ndoto ilikatika sehemu tamu, salamu zangu nawasilisha kwako. Nimeacha kwa Watanzania nao watume salamu zao. Naamini utapata muda uzisome ndoto zetu wote"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad