Mtatiro Afunguka Kuhusu Kuvuliwa Uanachama wa CUF

Mtatiro Afunguka Kuhusu Kuvuliwa Uanachama wa CUF
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro amekanusha habari zinazoenea kwamba amevuliwa uanachama wa chama hicho ambapo kwa upande wake amedai hilo ni tangazo la wahuni na wala haviwezi kumtingisha yeye.


Mtatiro amekanusha taarifa hiyo na kuifafanua kupitia mtandao wake maalum wa kijamii na kusema kuwa anaamini kuwa wanaosambaza taarifa hizo ni vijana wanaotumika ambao yeye kawaita 'wahuni'.

"Ndugu zangu, Nimeona taarifa kwenye mitandao kuwa kuna watu wanajiita viongozi wa CUF wilaya ya Ubungo na kwamba ati wamenivua uanachama wa CUF. Bila shaka hawa ni vijana wa Bwana yule na wanatumika kututoa kwenye ajenda kubwa za kitaifa," Mtatiro.

Aidha Mtatiro amefafanua kwamba taarifa za yeye kuvuliwa uongozi sizo za kwanza  hivyo haziwezi kumshughulisha, "Mwezi Disemba mwaka jana pia wahuni hao walitangaza ati wamenivua uanachama, tangazo lao la jana si jipya! Mimi naendelea na majukumu yangu kama kiongozi wa juu wa chama anayetambuliwa na chama na vikao vya chama, na vitangazo hivyo vya wahuni haviwezi kunishughulisha wala kuwashughulisha wenzangu".

Ameongeza "Nasubiri tangazo lingine la wahuni hao, la kunifukuza uanachama mara ya 3, ya 4, ya 5 na ya 6. Hawatushughulishi kabisa maana dawa ya mgonjwa ni kumpa dawa tu" Mtatiro.

Jana Jumapili Machi 4, 2018, Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ubungo, ndg.  Bashir Ally Muya, alitoa taarifa ya kumvua uanachama , Ndg Mtatiro ambapo alidai kwamba wamefikia uamuzi huo kutokana na Kiongozi huyo kukaidi agizo la chama hicho lililomtaka kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili, mbele ya baraza la utendaji la wilaya ya Ubungo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad