MTOTO mmoja mwenye umri wa miaka mitano amemfikisha katika Kituo cha Polisi Ngara, mkoani Kagera baba yake mzazi baada ya kubaini kuwa baba yake anataka kuuza kinyemela shamba ambalo ni urithi wa watoto wake.
Akizungumza baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo mwenye ujasiri mkubwa alikwenda kushitaki polisi kwa msaada wa dereva wa gari aitwae Thabiti aliyempa msaada wa lifti ya gari na kuhoji iwapoi baba yake atauza shamba, wao kama familia wataishi wapi?
Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni Baba, kukamatwa na polisi na kuhojiwa amekana kuhusu kutaka kuuza shamba hilo lakini mtoto amedai ni kweli baba yake alitaka kuuza shamba.
Alipoulizwa kama anafurahia baba yake kufungwa jela kwa kosa hilo alisema hafurahii baba yake kufungwa ikizingatiwa ana mzazi mmoja tu lakini alikuwa akipigania haki yake ya shamba kutokuuzwa kwani atakosa pa kwenda kuishi.
Kwa hakika mtoto huyu ni mfano wa kuigwa katika kupigania haki na usawa katika jamii.
Hutu Mtoto ni jasiri na anaakili za ziada zinazoweza kumuweka miongoni mwa watoto wenye vipaji maalum. Serikali na wahusika wadau wa maendeleo katika kuibuwa na kukuza watoto wenye uwezo maalum wa akili wanatakiwa kumtupia jicho huyu mtoto wasimuache akapotea hivi hivi tu. Ingekuwa tamu zaidi kama angekuwa mtoto wa kwanza kwenda kuonana na Raisi Magufuli kwani huyu Mtoto amesaidia kupambana na ufisadi kuanzia ngazi ya Familia ni kitu cha kupigiwa mfano.
ReplyDelete