Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.
Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi nibmaarufu kiasi gani."
"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.
Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo."
Diamond kamjibu kwa dharau kwakuwa ni mwanamke, tena ni binti mdogo anaweza hata 'kumtokea'.......mbona hakuwashambulia Basata ama TCRA amemshupalia Juliana....kama vipi ahamie nchi nyingine......watanzania tupo wengi mno, zaidi ya mil. 50......akitoka yeye hatutapungukiwa chochote......
ReplyDelete