Mwanamke Ajinyonga Hadi Kufa Kisa Bata

Mwanamke Ajinyonga Hadi Kufa Kisa Bata
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina Constansia James mkazi wa kijiji cha Kisorya, tarafa ya Nansimo wilaya ya Bunda, amejiua kwa kujinyonga baada ya tuhuma za wizi wa Bata.

Imeelezwa kuwa Marehemu aliiba bata huyo kwa jirani yake aitwaye Venaida Charles ambapo baada ya kufuatiliwa aligundulika yeye ndiye mwizi na aliamuriwa kulipa fidia kwa jirani yake, na ndipo alipoamua kujinyonga masaa machavhe baada ya hukumu hiyo.

Afisa Mtendaji wa kata ya Kisorya, Revocutus Luheneja amesema kifo hicho kimetokea juzi majira ya saa 10:00 jioni ambapo asubuhi ya siku ya tukio marehemu  Constansia (37) alituhumiwa kuiba bata na kutakiwa alipe fidia.

Luheneja amesema jirani huyo aliyeibiwa bata, alimkuta mnyama wake akiwa amechinjwa kwa muuza nyama na alipomuuliza aliyemuuzia, alimtaja marehemu Constansia na ndipo walipochukua maamuzi ya kumtaka alipe fidia.

“Venadia alichukua vifaranga vilivyoachwa na bata huyo aliyeibiwa na kwenda kwa wazazi wa marehemu Constansia kudai fidia, Lakini wakati wanaendelea kufanya taratibu za kulipana fidia, mwanamke huyo alipopata taarifa hizo alikwenda moja kwa moja ya musimu mkazi wa kijijini hicho aliyokuwa anataka kupanga na kuamua kujinyonga kwa kamba,“amesema Luheneja.

Kwa upande mwingine, Afisa tarafa ya Nansimo, Jonas Nyaoja amesema tukio hilo limesharipotiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Kisorya na mama aliyeibiwa bata huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad