Taarifa ya Sessions imeeleza kuwa McCabe amefukuzwa kazi kutokana na kuvujisha taarifa za uongo na kuwapotosha wapelelezi. Kigogo huyo wa FBI amekataa kuhusika na tuhuma hizo.
Ameeleza kuwa amezushiwa tuhuma hizo kwasababu alihusika katika kufuatilia suala la nchi ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016.
Rais Donald Trump amewahi kumtuhumu McCabe kuwa na upendeleo wa kisiasa kwa kuwa mfuasi wa Chama cha Democrats.