Hayo yameelezwa jijini Mwanza leo Machi 15 na mjumbe wa sekretarieti ya kuzuia na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, Ahmad Mwen-dadi wakati wa mafunzo maalumu kwa watekelezaji wa sheria za kupambana na usafirishaji wa watoto kwa ajili ya kazi za majumbani maeneo ya mijini.
Amewaeleza wajumbe wanaohudhuria mafunzo hayo yanayoratibiwa na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la Kiwohede, kuwa baadhi ya watoto wanaosafirishwa kwenda mijini kufanya kazi za ndani hujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na waajiri wao au ndugu wa familia wanakofanya kazi.
Mikoa mingine yenye idadi kubwa ya watoto wanaosafirishwa kwenda mijini kufanya kazi kwa mujibu wa Mwen-dadi ni Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Mafunzo hayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwohede, Justa Mwaituka yanahudhuriwa na askari polisi kutoka dawati la jinsia, watendaji wa idara ya mahakama, ofisi ya Mwanahseria Mkuu wa Serikali, Idara ya Uhamiaji, maofisa ustawi wa jamii na maofisa kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.