Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi Mkoani Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto iliyotokea mwaka jana ambapo amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na hatua za ujenzi zilipofikia.
Dk Nchemba amesema ameridhika na hatua iliyofikia katika ujenzi wa nyumba hizo ambazo ni za kisasa ambapo amedai kwamba hata polisi hao watakuwa wanajisikiam vyem kuishi katika nyumba hizo.
Aidha Waziri huyo mwenye dhamana ya mambo ya ndani ameshukuru hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huo uanze haraka pamoja Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wafanyabiashara wa Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo fikia kwa kusema kwamba walichukua hatua za mapema pale moto ulipotokea.
"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, hiili ni jambo kama waziri napaswa kumshukuru sana Rais kwani litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya," Dkt. Nchemba.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru Waziri Nchemba kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuwa karibu nao kati kipindi chote hicho, ambapo pia amemuomba Waziri Nchemba awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi Murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio ya kihalifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo na askari wanategemea gari linalotoka Kituo Kikuu cha polisi Arusha.