Mwigulu Amfananisha Abdul Nondo na Kinyango Aamua Kumchongea kwa Rais Magufuli

Mwigulu Amfananisha Abdul Nondo na Kinyango Aamua Kumchongea kwa Rais Magufuli
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kumwelezea Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kumfananisha kijana huyo na kinyago.


Mwigulu Nchemba alisema hayo Machi 11, 2018 akiwa mkoani Singida na kusema kuwa wapinzania wamekosa ajenda ndiyo maana wamekuwa wakihangaika kutafuta njama za kuchafua taswira ya nchi ya Tanzania.

"Mhe Rais ndiyo maana unaona vinyago vingi vingi hivi kama hivi juzi anatokea kijana mdogo eti anasema ametekwa, eti ametekwa akapata na muda wa kutafuta perfume na nguo za kubadilishia kule atakakokuwa ametekwa, unaotoa wapi muda wa kujiandaa ni vitu vya kiajabu ajabu kama hivyo watu wanatafuta namna za kuchafua taswira za nchi yetu na jambo hili si jambo ambalo tutacheza nalo" alisisitiza Mwigulu Nchemba

Mnamo Machi 6, 2018 mwanafunzi huyo aliripotiwa kutoweka katika mazingira tatanishi na siku iliyofuata yaani Machi 7, 2018 majira ya jioni ilisemekana kijana huyo alijikuta Mafinga ambapo alikwenda kuripoti kituo cha polisi, kisha baada ya hapo alisafirisha kutoka Iringa na kuletwa jijini Dar es Salaam kisha kukabidhiwa kwa Mkuu wa Upelelezi jijini Dar es Salaam (DCI) ambapo mpaka sasa upelelezi wa tukio lake unaendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad