Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harisson Mwakyembe pamoja na Baraza la Sanaa(BASATA) wametoa baraka kwa waandaji wa shindano la Miss Tanzania linalosimamiwa na The Look Company Limited, iliyopo chini ya Mkurugenzi wake, Basilla Mwanukuzi aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.
Baraka hizo zimetolewa katika ofisi ya Waziri ambapo alikutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Look Limited, Mwanukuzi ambaye amebeba dhamana ya shindalo hilo baada ya Mkurugenzi wa Kampuni wa Lino International Agency LTD Hashim Lundenga kutangaza rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo.
Miss Tanzania 2018 itazinduliwa rasmi April 7, mwaka huu na Mikoa 26 itahusika katika shindano hilo ambayo ni:- Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Kirimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Morogora, Mtawara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tabora, Tanga, Ilala, Kigamboni, Kinondoni na Temeke.
Febuari 28 mwaka huu, aliyekuwa Mkurungezi wa shindano hilo Hashimu Lundenga alitangaza kuacahana na shughuli za kuandaa shindano na kusimamia shindano la Miss Tanzania na alimpa kijiti cha kusimamamia na kuongoza kazi hiyo aliyekuwa Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi.