
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili yake ili kujua kama ana matatizo ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.
Leo ‘Nabii Tito’ hakuweza kufika mahakamani ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu Mwajuma Lukindo.
‘Nabii Tito’ anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe na anadaiwa kufanya hivyo Januari 25, 2018 akiwa mahabusu.