Mwanamuziki Alikiba atajwa kama mfano kwa wasanii wengine katika wasanii wanaotoa nyimbo zenye maadili ikiwemo upande wa audio na hata video zake huku akiisfiwa kuwa hajawahi kumba maneno yenye matusi au kutoa video yenye picha za watu wakiwa uchi , hivyo wasanii wengine washauriwa kuiga mfano wa msanii huyo.
Hayo yamesemwa jana tarehe 14 March na naibu waziri na baraza la sanaa walipokuwa wakifanya mahojiano na clouds media katika kipindi cha XXL, ambapo waliamua kufunguka na kusema sababu kubwa za kuwafungia wasanii wengi nyimbo zao.
"Kwa mfano Alikiba ni msanii mkubwa wa kimataifa na amekuwa akiwakilisha vyema nchi sehemu tofauti tofauti lakini mbona haimbi lugha chafu katika nyimbo zake wala video zisizokuwa na maadili .sisi kama wizara tunataka sanaa iende pamoja na ukuaji wa maadili ya nchi, tutoe burudani lakini tulinde utamaduni wetu." Aliongea Naibu Waziri Juliana Shonza.
Hivi karibuni wasanii zaidi ya kumi walifingiwa kucheza kwa nyimbo zao katika vituo vyote vya habari nchi , huku Roma akifungiwa kabisa kufanya kazi kwa muda wa miezi sita kutokana na sababu za kushindwa kufuata masharti ya kubadilisha wimbo wake wa kibamia. Download App Yetu >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !