Nape amefananisha kitendo hicho sawa na ushetani na kuwataka vijana wa Kiafrika kupambana kupinga mfumo huo ambao unakandamiza demokrasia.
“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa“amenena Mhe. Nape Nauye kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Rwanda tayari nchi hizo zimebadili mfumo wa ukomo wa urais madarakani ambapo Rais atahudumu kwa miaka 7 na Uganda wamefuta kabisa hadi ukomo wa umri wa Rais kustaafu.