Ndege za Tanzania Kuwasili Nchini Julai Mwaka Huu

Ndege za Tanzania Kuwasili Nchini Julai Mwaka Huu

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, amefunguka na kuweka wazi rasmi mwezi ambao ndege za Tanzania zitawasili nchini na kusema kuwa Julai mwaka huu ndege hizo zitaingia nchini.


Akiongea na waandishi wa habari leo Machi 5, 2018 Dkt. Abbas amesema kuwa ndege hizo zinategemewa kuingia nchini mwezi Julai na kudai kuwa ndiyo maana kumekuwa na nguvu kubwa ya kuendelea kufanya upanuzi wa viwanja vya ndege nchini ili kuruhusu ndege hizo kuweza kutua katika viwanja mbalimbali.

"Julai mwaka huu nchi yetu itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo 'Boeing Dreamliner' hivyo ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa/ Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi nchini" alisema Dkt. Hassan Abbasi.

Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbas amedai kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa maziwa makuu ya nchi yetu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria hivyo serikali imeanza mchakato wa kupata meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1200.

"Meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria  1200 na mizigo tani 400 Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwaka huu" Dkt. Hassan Abbas
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad