Ndoa za Utoto Zapungua Duniani

Ndoa za Utoto Zapungua Duniani

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo Machi 06, 2018 Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto ulimwenguni ( UNICEF) limesema kuwa kuna mafanikio makubwa ya kupungua kwa ndoa za utotoni duniani.

UNICEF wamekadiria kuwa ndoa za utotoni zipatazo milioni 25 zimeweza kuzuiliwa kwa kipindi cha muongo mmoja uliyopita.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa msichana mmoja kati ya watano anaolewa chini ya miaka 18 tofauti na miongo iliyopita ambapo ilikuwa msichana mmoja anaolewa kati ya wanne.

UNICEF wamesema bara la Asia hususani Asia ya Kusini limejitahidi zaidi katika kupunguza ndoa za utotoni, ambapo ripoti imesema wamepunguza kwa asilimia 20 kutoka 50 iliyokuepo miaka 10 iliyopita.

Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNICEF, Anju Malhotra amesema kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na sera nzuri za serikali ikiwemo elimu kwa watoto juu ya ndoa za utotoni.

“Kama msichana atalazimishwa kuolewa akiwa mtoto, atkabiliwa na madhara makubwa siku za usoni. Kwani itakuwa ni kikwazo kwa kupata elimu pia ni rahisi kudhalilishwa na mumewe na inahatarisha maisha kipindi cha kujifungua. Mbaya zaidi ndoa za utotoni zina madhara makubwa kwenye jamii ikiwemo umasikini.”amesema Bi. Malhotra.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa nguvu kubwa ya kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni imehamia barani Afrika,ambapo jitihada za ziada zinahitajika ili kupunguza tatizo hilo.

Soma ripoti hiyo kamili iliyotolewa na UNICEF ->25 million child marriages prevented in last decade due to accelerated progress, according to new UNICEF estimates
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad