Baada
ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kutaja hadharani dosari
kumi zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo uliofanyika kwenye majimbo ya
Kinondoni na Siha, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
Kailima Ramadhani amedai kuwa kituo hicho kimefanya makosa.
Alisema kituo hicho kimetangaza dosari hizo za uchaguzi uliofanyika Februari 17, bila kufuata sheria na kanuni za uchaguzi.
Uchaguzi
huo ulifanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo, Maulid
Mtulia (CUF-Kinondoni) na Dk Godwin Mollel (Chadema-Siha) kujitoa kwenye
vyama vyao na kuhamia CCM.
Wabunge hao wawili waliopitishwa tena kwenye uchaguzi huo kupitia CCM walishinda nafasi hizo.
Kutokana na uchaguzi huo, LHRC ilitoa dosari zilizofanana na zile zilizotolewa na vyama vya upinzani hasa Chadema.
Akizungumza
wakati wa mahojiano na kituo cha Magic FM, Kailima alisema LHRC
imefanya kosa la kisheria na kanuni kwa kutoa taarifa hiyo.
Alisema
kifungu namba 4 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeielekeza tume hiyo
kutunga kanuni wakati kifungu namba 64(4) cha Sheria ya Taifa ya
Uchaguzi kinasema Tume itatoa muongozo kwa watazamaji wa uchaguzi.
Alieleza kwamba hata katika uchaguzi wa mwaka 2015, tume hiyo ilitoa muongozo kwa watazamaji wa uchaguzi.
“Kipengele
cha 12(d) kinasema mtazamaji hatatakiwa kutoa taarifa kwa umma juu ya
mchakato wa uchaguzi hadi taarifa ya awali itakapokuwa imekabidhiwa na
tume kukiri kupokewa kwa taarifa hiyo,” alisema Kailima.
Alifafanua
kuwa kituo hicho kiliandika barua kwa tume na kuiwasilisha Februari 26
ambayo iliifikia tume Februari 28 jioni wakati ofisini kukiwa hakuna
viongozi.
“Kutozingatia sheria ni kama wembe, utakukata tu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema tume hiyo inatafakari iwapo itawapa kibali kingine cha utazamaji wa uchaguzi.
Kuhusu
hoja zilizo kwenye taarifa hiyo ikiwamo ya matumizi ya watoto kwenye
kampeni za chama kimojawapo, Kailima alisema wao si Wizara ya Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto na kwamba hoja hizo ilipaswa zipelekwe huko.
Hawa LHRC kwanini wasijisajili kama chama cha siasa? Wajiandikishe tu kuwa miongoni mwa cha chama shiriki kwenye umoja wa ukawa. Na kwanini siku zote huuelekeza hicho leo kuyaona mapungufu ya upande moja tu yaani serikali na chama chake tawala? Ukweli ni kwamba hakuna kitu kinachowakosesha haki za msingi za kibinaadamu Watanzania kama hali duni ya maisha inawakabili iliyosababishwa zaidi na vitendo vya rushwa na ufisadi kitu amabacho serikali iliopo madarakani imepigana na kupambana na kuendelea kupambana kufa kuhakikisha watanzania wanaondakana na umasikini pamoja na kulindwa haki zao za msingi zilizokuwa zikibanwa na masuala ya kifisadi ambapo vyama pinzani wanaotetewa na hiyo taasisi inayojiita ya kutetea haki wamekuwa wapingaji wakubwa na kuendesha hujuma za wazi kuhakikisha serikali iliyopo madarakani inashindwa kuwaletea watanzania maendeleo. Au kazi za kutetea haki za binaadamu madhumuni ya kuwepo kwake ni kuunga mkono upinzani tu hata kama wao wenyewe binafsi ndani ya vyema vyao hawatendeani haki ndani? Maana Mwenyekiti Mbowe ni Dikteta wa wazi ndani ya chama chake hao watu wa haki za binaadamu wapo wapi?
ReplyDelete