Nikki wa Pili Atoa Ujumbe Mzito Kuhusu Viwanda

Image result for Niki wa Pili
Msanii Niki wa Pili ameitaka serikali inapotekeleza sera ya viwanda ihakikishe inajenga na kiwanda kila mkoa kwa ajili ya kutengeneza taulo za kike (pads), ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua.




Akiungana na East Africa Television, East Africa Radio na Msichana initiative, Nikki wa Pili amesema ni vyema kwenye kila viwanda 100 ambavyo vinatarajiwa kujengwa kwenye kila mkoa kama serikali inavyokusudia, ni vyema wakaweka kiwanda kimoja kwa ajili ya kutengeneza vitaulo vya kike.

“Kila mwezi binti anaenda kwenye siku zake, na tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya mabinti ambao wako sekondari hawana uwezo wa kununua pedi na kusababisha kukosa shule wakati wa kipindi cha mzunguko wa hedhi, jambo ambalo linampunguzia nguvu za kujiamini na kumuathiri kisaikolojia. Kuna kampeni ya kuhamasisha kujenga viwanda 100 kwa kila mkoa, kwa nini kwa kila viwanda mia tunavyotaka kujenga, tusijenge kiwanda kimoja tu cha kutengeneza pedi na kuwasaidia mabinti, hii itamsaidia kumjengea uwezo pia”, amesema Nikki wa Pili.

East Africa Television, East Africa Radio na Msichana Initiative, inaendesha kampeni ya #Namthamini kwa ajili ya kuchangisha pedi kwa ajili ya kuwasaidia wanafunbzi wa kike ambao hawana uwezo wa kununua bidhaa za kujisitiri wanapokuwa kwenye siku zao, ili waweze kubaki darasani na kuendelea na masomo bila kipingamizi chochote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad