Nyota ya Wastara Yang'aa Apata Shavu Sweden

Wastara Apata Shavu Sweden
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ambaye hivi karibuni alikuwa nchini India kwa matibabu, baada ya kurudi Bongo na kupata nafuu amelamba shavu la kwenda nchini Sweden kuwakilisha wanawake walemavu wa Kiafrika.



Akiongea na Risasi Jumamosi juzi, Wastara alisema kuwa baada ya kutua nchini akiendelea na matibabu alipata mwaliko wa kwenda Sweden kwa ajili ya kuwawakilisha wanawake walemavu baada ya kuchaguliwa na Jumuiya ya Wanawake Afrika yenye makao yake makuu nchini Swenden akiwa kama balozi wa wanawake kutoka Tanzania.

“Nimelazimika kwenda kwa sababu hakuna mwanamke mwenye historia kama ya kwangu na wamenihakikishia kuwa nitakuwa salama kuanzia kwenye safari mpaka huko kwani bado nipo kwenye matibabu,” alisema Wastara



Mbali na safari hiyo, Wastara pia amezindua wimbo wa kuwashukuru Watanzania wote waliomchangia pesa za matibabu ambao umeimbwa na msanii ‘anayemmeneji’ aitwaye Kea.

“Nimeamua kuwashukuru Watanzania kwa kutumia mashairi ikiwa ni pamoja na kuwaburudisha lakini kubwa ni kuwashukuru kwani leo hii nilivyo ni kwa sababu ya wao, bila kumsahau Rais Magufuli,” alisema Wastara. Wastara alikwea pipa juzi kuelekea Sweden ambapo atakaa kwa siku chache.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad