Ombea Mumeo Asifanikiwe na Kuwa Tajiri...Ugumu wa Maisha Ndio Unamfanya Akupende

Kwa jamii zetu za kiafrika nilikua nikiamini kwamba familia yenye amani,furaha na upendo ni ile yenye mafanikio na uhuru wa kifedha. Ila kadiri ninavyozidi kukua najiona sikua sahihi pale ninapoona mambo yanayotokea kwenye jamii yangu. Wanawake wengi ambao waume zao wana fedha wanalia na kusaga meno.

Binti ikitokea mumeo anakupenda na kukujali basi ombea sana hiyo mbuzi isifanikiwe,kwani tabia halisi ya mwanaume huonekana pindi anapopata fedha. Unaweza ukadhani anakujali kumbe ni ugumu tu wa maisha ndio unaomfanya awe mnyenyekevu kwako ila hela zikimchanganyia my dear utalazwa chini na kimada atalala kwenye kitanda chako.

Nimeshuhudia wanaume waliooa wakiwa na "official michepuko" yani mtu kafunga ndoa kwenye nyumba ya ibada ila ana binti pembeni ambae familia na mkewe wanamjua na anafanya makusudi kwa kua ana fedha na familia inamtegemea yeye.

Kwa tabia hizi blaza usitegemee hata siku moja kusikia mkeo akikuombea ufanikiwe zaidi kwa sababu anajua fika ya kwamba hatua moja zaidi ya mafanikio ni sawa na wewe kuongeza mwanamke mwingine wa nje official hivyo siku zote maombi yake yatakua ni kukuombea ili ufilisike na heshima kwa mkeo na familia irudi.

Ukimheshimu mkeo na familia yako basi waheshimu katika hali zote. Usijione wewe ndio master planner ukadhani mafanikio uliyo nayo ni juhudi zako pekee. Hakuna kisicho na manufaa duniani kwani hata saa mbovu hua sahihi mara mbili kwa siku.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad