Operesheni Kumg'oa Mugabe Yaibua Mambo Mazito


Operesheni Kumg'oa Mugabe Yaibua Mambo Mazito
Matokeo ya uchunguzi wa Baraza la Taifa la Ukimwi (NAC) na Jeshi la Polisi la Zimbabwe (ZRP), unaonyesha kuwa maofisa wa jeshi la Wananchi wa Zimbabwe wanadai huduma ya ngono bure kutoka kwa wanawake wanaojiuza kama shukrani kwao kwa kusimamia 'Operesheni Rejesha Heshima', Novemba mwaka jana.

Uchunguzi huo uliofanywa mwezi uliopita baada ya operesheni hiyo iliyomuweka madarakani, Emmerson Mnangagwa ulilenga kupima uelewa wa maofisa wa polisi, tabia zao na ushiriki wao katika ngono, ushoga na matumizi ya dawa za kulevya.

Wakati wa utafiti huo, wanawake hao wanaojiuza waliwalalamikia wanajeshi kwamba baadhi yao wamekuwa wakitumia bunduki kuwatisha, ili wafanye nao ngono bure.

"Wanajeshi wamekuwa wasumbufu katika baadhi ya maeneo kwani wanataka ngono bure hasa baada ya kushiriki katika Operesheni ya Kurejesha Heshima,” inasema taarifa ya utafiti huo huku ikitaja matukio kuwa mengi zaidi kutokea katika eneo la Chiredzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad