Picha: Hivi Ndivyo Polepole Alivyonusurika Kufa Baada ya Msafara Wake Kupata Ajali

Picha: Hivi Ndivyo Polepole Alivyonusurika Kufa Baada ya Msafara Wake Kupata Ajali
Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba T150 EWE iliyokuwa ikiendehswa dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hosiptali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Poplepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mara ya ngapi hii gari za viongozi wa CCM zinapata ajali kwa kupasuka matairi ziarani? Lazima kutakuwa na mchezo machafu unafanyika na kwa kweli wanaotekeleza ushenzi huo hawaitakii mema Tanzania. Pole pole mpende usimpende lakini ni moja kati ya watu makini sana na mahiri katika masuala ya siasa. Sio hazina kubwa ya kisiasa kwa CCM TU bali kwa taifa kwa ujumla na kitendo cha kutaka kummaliza kinafaa kulaniwa na ni matumaini yakwamba uchunguzi wa wa kina utafanyika kubaini wahusika.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad